- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Barbados, Trinidad & Tobago:Plastiki na Uchafuzi wa Mazingira

Mada za Habari: Nchi za Caribiani, Barbados, Trinidad na Tobago, Harakati za Mtandaoni, Mazingira, Sheria

“Fanya matembezi kwenye pwani yoyote nchini Barbados – na utaona uchafu wa plastiki uliosukumwa ufukweni”: Barbados Free Press [1] anauliza kama uuzaji wa chupa za plastiki za maji uwekewe vikwazo, wakati Mtrinidadi Keith Francis [2]pia anaguswa na suala la uchafuzi wa mazingira kwa plastiki ulimwenguni.