Habari kutoka 23 Disemba 2009
Singapore: Kampeni ya “Kataa Ubakaji”
Nchini Singapore, mara nyingi kumbaka mke wako hakuchukuliwi kama tendo la kubaka. Waandaji wa kampeni ya “Kataa Ubakaji” wanataka kukomesha sheria inayokinga ubakaji ndani ya ndoa kwa kuzindua kampeni ya kukusanya saini ambazo zitawasilishwa kwa watunga sera. Wengi wa raia wa mtandaoni wanaiunga mkono kampeni hii.
Misitu ya Madagascar Inateketezwa kwa $460,000 kwa Siku
Wakati mataifa ya dunia yanakutana huko Copenhagen kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, Madagascar, ambayo imekwishapoteza 90% ya misitu yake ya asili, inakabiliwa na tishio la biashara ya magendo ya magogo, inayotishia kuharibu kile kilichobakia katika moja ya mifumo ya mazingira yenye viumbe na mimea mingi inayotofautiana.
Ethiopia: Meles Zenawi aisaliti Afrika
Lucas Liganga aandika kuhusu usaliti wa Waziri Mkuu wa Ethiopia: “kwa bahati mbaya, Waziri Mkuu wa Ethiopia meles Zenawi ambaye ni msemaji wa Afrika kuhusu mabadiliko ya tabianchi amejiunga na...