6 Disemba 2009

Habari kutoka 6 Disemba 2009

Guinea: Jaribio la Kumuua Kiongozi wa Kijeshi Dadis Camara

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, Kapteni Dadis Camara, kiongozi wa kikundi cha jeshi kilitwaa madaraka nchini Guinea mwezi Disemba 2008, alipigwa risasi na kujeruhiwa na mmoja wa wasaidizi wake jana mjini Conakry. Wasomaji wengi wa RFI wanaodai kuwa Camara anawajibika kwa mauaji ya waandamanaji wa upinzani yaliyotokea tarehe 28 Septemba, wanaoana kuwa haki imetendeka.

Guatemala: Kuvunja Milango ya Madanguro

  6 Disemba 2009

Blogu inayojulikana kama Noticias para Dios inatoa habari za ndani, kama vile mambo yenyewe yanavyotokea pasipo kuficha kitu, kuhusu maisha ya kila siku ya mwanasheria wa Ki-Guatemala anayejaribu kuwaokoa watoto kutoka kwenye madanguro ambako wamekuwa wakiishi baada ya kuchukuliwa kutoka makwao.

Mchakato wa Amani Nepal Unayumba

  6 Disemba 2009

Mchakato nyeti wa kuleta amani nchini Nepal unasitasita katikati ya mapambano yanayozidi kuongezeka kati ya watu wa kundi la ki-Mao na serikali. Kundi la ki_Mao linatishia kuitisha mgomo usio na kikomo kama madai yao hayatatekelezwa.