- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Yoani Sanchez Pamoja na Wanablogu Wengine wa Cuba Wakamatwa na Kupigwa

Mada za Habari: Amerika Kusini, Cuba, Habari za Hivi Punde, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Uhuru wa Kujieleza

Jioni ya tarehe 6 Novemba, blogu ya Babalú iliweka kiungo [1] kuelekea makala [2] iliyoandikwa na Penultimos Dias (es) ilitoa taarifa kuwa baadhi ya wanablogu mashuhuri wa Cuba, wakiwemo Yoaní Sánchez na mchangiaji wa Global Voices Claudia Cadelo, walitiwa mbaroni na majeshi ya usalama. Habari mpya kutoka kwa Penultimos Días zinataarifu kuwa Sanchez na Orlando Luis Pardo “walipigwa vibaya na kutukanwa”.