- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Misri: Mwanablogu wa Kiume Aagizia Bikra ya Bandia

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, China, Misri, Dini, Haki za Binadamu, Mawazo, Sanaa na Utamaduni, Wanawake na Jinsia

Wakati Redio ya Uholanzi [1] ilporusha hewani tafsiri ya Kiarabu kuhusu Zana ya Kutengeneza Bikira ya Bandia, pale gazeti la Youm7 [2] lilipotangaza kuwa bidhaa hiyo itaanza kupatikana kwenye soko la Misri, wabunge wahafidhina huko Misri walitaka bidhaa hiyo izuiwe na muagizaji yeyote afukuzwe nchini au akatwe kichwa [3], na habari hiyo ilipozua kelele kwenye ulimwengu wa blogu wa Misri [4], Mohamed Al Rahhal [5] alinunua zana hiyo maalum ya kutengeneza bikira ya bandia.

Wakati alipokwenda kuchukua kifurushi chake ofisi ya posta:

Nilikuta kimeshafunguliwa na maafisa mbalimbali wa forodha na posta ambao, baada ya kukosa majibu, waliandika utambulisho wa bidhaa hiyo kama “yenye majimaji mekundu yasiyofahamika” – na walisubiri maelezo yangu.

Aliwaeleza kuwa ni “vipodozi vya wacheza sinema” na kuichukua bidhaa ile nyumbani:

Hiyo ndiyo “bikira”: kipande kilichokunjwa cha plastiki cha sentimeta 5×7 – cha ute wa protini unaoitwa albumin, maelezo yalinisahihisha kwa haraka – kilichopakwa wino mwekundu kwenye upande mmoja. Kikiwekwa ukeni kabla ya kujamiiana, plastiki hiyo huganda kidogo, na hupasuka wakati wa tendo. Matone machache ya “damu” huchafua shuka, na kutunza “heshima” ya mwanamke, familia yake au jamii yake.

Kama fanya kazi au la siwezi kujibu. Kutokuwepo kabisa kwa maelezo ya kitaalamu kwenye bidhaa hiyo, pamoja na shutuma mtandaoni kuwa bidhaa hii inaweza kusababisha magonjwa, vilinifanya nisite kumpoatia mtu atakayejitolea kufanya jaribio.

Mona El Tahawy hakupendezwea na jinsi Wamisri walivyopamba moto na kuguswa [6] juu ya bikira bandia pamoja na matatizo yote Wamisri wanayoyakabili siku hizi – gharama za maisha zinazopanda, rais aliye madarakani kwa miaka 28 ambaye mwanawe anaelekea kumrithi, nk. – kelele zote za nini juu ya bikira, iwe ya kweli au ya bandia?

Karibuni kwenye unafiki na kujidanganya ambavyo kwa pamoja vinadunda katikati ya roho mitazamo ya kihafidhina ya kidini juu ya wanawake na uadilifu katika kufanya mapenzi. Na katika shauri la Misri, uhafidhina huo upokatika mizani sawa kote, kwa Waislamu na Wakristu.

Kama Muislamu, ninajua kuwa Qur’an inahubiri uadilifu katika kufanya mapenzi kwa wanaume na wanawake, lakini kushupaliwa huku kwa wanawake na wahafidhina kunamaanisha kuwa ni wanawake tu ambao wanatarajiwa kuzingatia makatazo juu ngono nje ya ndoa. Huku kushupaliwa kwa bikira kumekosa kina zaidi ya yote na kuna hali ya umauti zaidi.

Mohamed El Rahhal anashutumu vikali:

Unafiki ambao unaturuhusu kubagua dhidi ya asilimia 50 ya jamii wakati tunatoa kibali cha bure kwa nusu nyingine. Ninapinga kuwalazimisha wanawake kwenda umbali huo, mara nyingine kuhatarisha afya zao, ili kuruhusu kucheleweshwa kwa sheria ya kitaifa juu ya mahusiano ya kijinsia.

Uadilifu unatafsiriwa vibaya zaidi na maumbile. Na kama tunasubiri kipande kidogo cha plastiki kifafanue uadilifu, basi tumeshashindwa – na ni budi tutafute ufafanuzi mzuri zaidi.