- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Ghana: Vionjo Sehemu ya Kwanza

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Ghana, Historia, Safari, Sanaa na Utamaduni

Sehemu ya kwanza ya vionjo vya Ghana [1]iliyotayarishwa na Gayle: Nchini Ghana, kila kanda ina kitu cha kutoa. Utamaduni, historia, pwani, wanyama na mimea, unaweza ukavivinjari nchini kote, kutokea kwenye mitisitu ya kitropiki kule kusini mpaka mbuga za savana za kaskazini. kama ni mpenzi wa pwani au historia, utaburudika na ziara hii ya sehemu za pwani.