Georgia: Aibu Katika Kanisa la Orthodox

Katika nchi inayofuata dini zaidi kwenye maeneo ya kusini mwa Caucasus ambako mkuu wa Kanisa la Orthodox (madhehebu ya Kanisa la zamani au kihafidhina) anaweza hata kuhamasisha ongezeko la watoto, kukosoa watumishi wa kanisa bado ni mwiko. Kuwatania, hata hivyo, ni jambo baya zaidi na lililojaa hatari, kama blogu hii ya This is Tbilisi Calling inavyoripoti.

Askari polisi wa Georgia wanaripotiwa kuwa wameweza kuwafuatilia na kuwapata waharibifu wa fikra waliohusika katika utengenezaji wa video za masihara ‘chafu na zinazotusi’ ambazo zilimlenga mkuu wa Kanisa la Orthodox na kusababisha aibu katika taifa zima kwenye nchi hii yenye kufuata dini kwa bidii. Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani iliwatambua wakosefu hao kuwa ni mwanafunzi wa shule ya msingi na mwanafunzi mwingine mkubwa. […]


Evolutsia
, anaangalia suala kubwa zaidi linalohusiana na nguvu za Kanisa pamoja na uhuru wa maoni. Katika makala ya maoni kwenye blogu mpya ya habari kwa lugha ya Kiingereza iliyozinduliwa, Inge Snip anapiga kengele za tahadhari.

Moja ya uhuru wa msingi, ninaamini, ni uhuru wa maoni. Uhuru wa maoni unawezesha nchi kumuonyesha kila mwananchi wake kuwa maoni yao yanaruhusiwa kusikilizwa, bila kujali yaliyomo. Na kwa kuongeza, demokrasia ya kweli inaruhusu kutaniwa kwa watu muhimu kwenye jamii, na kwa kufanya hivyo, inaonyesha kukomaa kwake.

[…]

Na kwa kumalizia, hakuna sababu ya kuchunguza suala hili, na wala haipaswi kuwepo; hata hivyo, vyombo vya kutunza sheria vilifanya kinyume, kwa sababu kuna namna fulani ya matakwa ya wengi. Kama mwanafunzi wa sheria, kwa urahisi, hii ni moja ya sababu za kijinga katika uchunguzi wowote wa kisheria ambao nimewahi kuusikia.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.