- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Cuba: Ukweli wa Sanchez Kutiwa Mbaroni Waibuka

Mada za Habari: Amerika Kusini, Cuba, Habari za Hivi Punde, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Uhuru wa Kujieleza

Kukamatwa, kupigwa na kuachiwa huru kulikofuata kwa wanablogu Yoaní Sánchez, Claudia Cadelo na Orlando Luis Pardo kulikofanywa na majeshi ya usalama ya Cuba tarehe 6 Novemba, kunapata matangazo mengi katika vyombo vikubwa vya habari [1] na katika ulimwwengu wa blogu pamoja na ule wa Twita. Yoani ameandika [2] (es) kuhusu tukio hilo kwenye blogu yake, Generación Y, na blogu za Kiingereza kama vile Babalú Blog [3], Repeating Islands [4] pamoja na Uncommon Sense [5] zinafuatilia habari hiyo. Mahojiano ya sauti [6] (es) na Sanches kuhusu tukio hilo yamepandishwa kwenye YouTube.