Algeria-Misri: Ugomvi Juu ya pambano la Mpira kwenye Mtandao

Hali tete kati ya mashabiki wa mpira wa miguu wa Misri na Algeria inazidi kukua kabla ya pambano litakalofanyika mjini Cairo tarehe 14 Novemba. Mchuano huo utaamua ipi kati ya timu hizo zitafaulu kwenda kwenye Kombe la Dunia la FIFA Afrika ya kusini mwaka ujao. Misri inahitaji japo ushindi wa magoli mawili ili kulazimisha mchezo wa kukata shauri katika uwanja wa nchi nyingine ambapo Algeria, ambayo imeshindwa kufaulu kwenda kombe la dunia tangu 1986, itapambana ili kutunza nafasi yake ya sasa ya kuongoza katika kundi la wanaogombania nafasi ya kufaulu. Wakati wa kuelekea pambano la Jumamosi, mashabiki washindani wamekuwa wakijiandaa nje ya mtandao wa intaneti, kadhalika katika malumbano makali ya mtandaoni, ambayo yamekua na kugeuka “vita-vya-mikwara-kwenye-mtandao”

Mwanablogu wa Algeria Adel [Fr] anatoa muhtasari wa mlolongo wa matukio ambayo yamesababisha mzozo. Anaandika:

Ce n’est pas sur le carré vert que le match a commencé à se jouer mais sur la toile. En attendant l’entrée des 22 joueurs sur la pelouse du fameux Cairo Stadium, la rencontre a débuté de manière assez peu banale entre les «Facebookeurs» (membres du réseau Facebook) algériens et égyptiens. Tout a commencé par de simples discussions dans les forums avant que cela ne prenne de l’ampleur. Voulant montrer leur savoir-faire dans la retouche d’image, les Egyptiens ont été les premiers à ouvrir les hostilités en publiant des photos «anti-algérien».

Les Egyptiens voulaient expliquer à travers un tel acte que leurs joueurs sont «très forts» et qu’ils sont en mesure d’écraser l’équipe nationale algérienne. Cela donna le top à une guerre d’un genre particulier. La guerre des images et des parodies.

Inaelekea kuwa mechi imeshaanza mtandaoni, mbali na uwanja wa mpira. Kabla ya wachezaji 22 kuingia uwanja maarufu wa Cairo, pambano kali limeanza katik ya watumiaji wa Facebook wa Kialgeria na Kimisri. Yote yalianza na majadiliano ya kirafiki katika majukwaa ya mtandaoni, kabla ya mambo kuzidi kipimo. Wakitaka kuonyesha utaalamu wao wa kuhariri picha, Wamisri ndio walikuwa wa kwanza kuanzisha uhasama kwa kuchapisha picha “zinazoipinga Algeria”.

Wamisri walitaka kuonyesha kuwa wachezaji wao ndio “wenye nguvu” na kwamba wana uwezo wa kuiponda timu ya taifa ya Algeria. Hii ilitoa ishara ya kuanza vita ya namna ya pekee. Vita ya picha na utani.

Video, zilizoiga picha zilichokuliwa kutoka kwenye filamu maarufu za Hollywood, zilifurika kwenye YouTube, na kuweka ugomvi huu katika ngazi ya…..

Katika video inayofuata [Ar], iliyowekwa na hakemvoip [Fr], Mel Gibson ni Rabah Wallace (Katika filamu ya Braveheart), jemedari wa vita wa Kialgeria ambaye anajaribu kuhamasisha wapiganaji kabla ya vita inayotarajiwa:

Katika video hii, Mmisri ulyesis anawakaribisha mashabiki wa Algeria katika kile anachokiita “jehanam” ndani ya jiji la Cairo:

Mwanablogu GEMYOoOD [Ar] katuma picha ya maelfu ya mashabiki wa Misri waliopanga foleni katika sehemu tofauti za Cairo, wakitarajia kupata tiketi kwa ajili ya mechi. Anachapisha picha za mikusanyiko hiyo ya watu:

GEMYHOoOD pia anatuma baadhi ya maoni ya watu wanaoshuhudia:

انا خدت اجازة اليوم ونزلت من الصبح لنادي الصيد الساعة 8 الصبح وللاسف لقيت موت ناس وزحمة وطابور فيه حوالي 3000 واحد ودفع وشتيمة والناس كل شوية بتزيد ومش عارف اقف من الزق والعرق بجد مهزلة

Nilichukua ruksa ya siku ili nije kwenye klabu saa 2 asubuhi [kununua tiketi]. Kwa masikitiko nilikuta kundi kubwa la watu na foleni kubwa ya kadri ya watu 3000, huku watu wakisukumana na kutukanana. Sikuweza kusogea. Nilikwama. Nikafikiri, hiini aibu.

Basi rasmi la timu ya mpira wa miguu ya Algeria, ambalo liliwasili mjini Cairo tarehe 12 Novemba, inadaiwa kuwa lilishambuliwa na mashabiki, kama video inayofuata, iliyotumwa katika YouTube na Vidéos Mouloudia Club d'Oran, inavoelekea kuonyesha:

Baraza linalodhibiti mpira wa miguu duniani FIFA, lilihisi umuhimu wa kutoa onyo kwa vyama vya mpira wa miguu vya Algeria na Misri, likiwakumbusha wote kuwa “mashindano ya awali kwa ajili ya kombe la Dunia 2010 yamalizike kama yalivyoanza, katika moyo wa mchezo wenye haki ulio na ushirikiano unaohitajika kutoka kwa washiriki wote.”

Tovuti, Algerie Egypte Match [Ar, Fr], inayoandika kuhusu tukio hili na kufuatilia kila namna ya habari inayohusiana na mechi, iliundwa na washabiki wa Algeria.

Katika hali hii ya ushindani mkali, baadhi ya watu wameunda kundi kwenye tovuti ya mtandao wa kijamii Facebook, wakiomba hisia mbaya zaidi. Laama Bouchema katuma ujumbe katika ukuta wa kundi hilo unaosema:

Pamoja na kukasirika kwangu kutokana na kilichoitokea timu ya Algeria, siihukumu nchi yote kwa kile alichofanya mpumbavu mmoja! Wanachokifanya mashabiki wenye hasira ni upumbavu! kwa ajili ya mungu si jambo kubwa ni nani atakeyeingia katika [kombe la dunia].

Mwanablogu wa Kimisri Lasto Adri [Ar] anaeleza kuchukizwa kwake na jinsi kile kilichopaswa kuwa tukio la michezo, kimeshushwa hadhi na kuwa pambano chafu. Anaandika:

مندهشة من التعصب وتدنى مستوى لغة الحوار بين مشجعى منتجب مصر ومنتخب الجزائر والظاهر بوضوح فى التعليقات على المواقع الإخبارية أو الرياضية… ومندهشة أكثر بتغذية هذه المأساه إعلاميا بتعليقات من بعض المذيعين (من كلا الجانبين)…
المشجعون الجزائريون أخطؤوا فى المبارة السابقة.. لكن هل الرد يكون هكذا؟.. هل الرد يكون بطلب البعض تسميم اللعيبة ولا إقلاقهم فى منامهم ولا توليع الإستاد وقت الماتش من التشجيع؟..
ونرفزتنى التعليقات على أغلب المواقع.. وإفتكرت لما الجزائر -بزعامة الرئيس الجزائري هواري بومدين- كانت أكتر دولة ساندت مصر فى حرب 1973، رغم فقرها الشديد..
حزينة ان انتهاء علاقة مابين شعبين تكون بشقاق على كورة…

Ninashangazwa na kiwango cha kutovumiliana na lugha chafu inayotumiwa na mashabiki wa timu za Algeria na Misri, ambayo inajitokeza katika maoni mengi kwenye tovuti za habari na michezo… pia ninashangazwa na jinsi ambayo baadhi ya watangazaji na wanahabari (kutoka pande zote), wanavyochochea dhahama hii kupitia maoni yao makali…
Mashabiki wa Algeria hawakujiheshimu katika mchezo uliopita… lakini je jibu la Wamisri ni sahihi?..
Je jibu linapaswa kuwa (kama baadhi walivyosema) kuwapa sumu wachezaji wa Algeria? Kuwaghasi na kuwanyima usingizi? Kuuchoma moto uwanja siku ya pambano?
Nimeudhika na maoni yaliyo kwenye tovuti nyingi… Ninakumbuka wakati Algeria – ikiongozwa na Rais Houari Boumedienne – bila kujali umaskini wao uliokithiri, alikuja kuiunga mkono misri wakati wa vita ya mwaka 1973…

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.