Habari kutoka 11 Novemba 2009
Video: Dunia Yaadhimisha Kuanguka kwa Ukuta wa Berlini
Leo ni Kumbukumbu ya 20 ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlini, kizingiti madhubuti cha kiusalama ambacho kiliwahi kuligawa jiji la Berlini katika pande mbili za Mashariki na Magharibi huko Ujerumani. Leo tunaonyesha baadhi ya picha za video zinazotoka pande mbalimbali za dunia zinazopandishwa ili kusherehekea siku hii na nini ukuta huo ulimaanisha siyo Ujerumani tu bali duniani kote.
Afrika Kusini: Wimbo wa Taifa kwa Wanaoongea Kiingereza
Wimbo wa Taifa wa Afrika Kusini kwa wanaoongea Kiingereza: Ni njia kuu iliyoje ya kufafanua kwa kuonyesha Wimbo wa taifa wa Afrika Kusini kwa wale kati yetu ambao kwanza hatuufahamu...
Naijeria: Wanablogu Wajadili Sifa Mbaya ya Naijeria
Inajulikana vyema kuwa Naijeria ina tatizo la muonekano – utapeli wa 419 kwenye intaneti, rushwa, uharamia wa mafuta katika jimbo la Delata – kwa watu wengi, huu ndio uhusiano unaokuja akilini wakati nchi yenye watu wengi zaidi Afrika inapotajwa.