Habari kutoka 4 Novemba 2009
Georgia: Aibu Katika Kanisa la Orthodox
Katika nchi inayofuata dini zaidi kwenye maeneo ya kusini mwa Caucasus ambako mkuu wa Kanisa la Orthodox (madhehebu ya Kanisa la zamani au kihafidhina) anaweza kuhamasisha ongezeko la watoto, kukosoa watumishi wa kanisa bado ni mwiko. Kuwatania, hata hivyo, ni jambo baya zaidi na lililojaa hatari.
Kenya: Ramani Mpya Ya Wazi ya Kitongoji Cha Kibera Kwenye Blogu
Mradi wenye lengo la kutengeneza ramani mpya ya wazi ya kitongoji cha Kibera mjini Nairobi, Kenya: “Na jana tulimaliza siku nzima pale MS Action Aid kenya, ambako wanafunzi wa ki-Denmark...
Iran: Majeshi Ya Usalama Yawashambulia Waandamanaji
Kwa mujibu wa Kian majeshi ya usalama yaliwashambulia waandamanaji katika viwanja vya hafteh tir mjini Teheran na kuwajeruhi watu kadhaa.
Misri: Watu 10 Wenye Ushawishi Zaidi Nchini
Mtoto wa Rais wa Misri, Hosni Mubarak, anayitwa Gamal Mubarak, -- na ambaye anatarajiwa kumrithi baba yake nafasi hiyo -- aliibuka kama mmoja wa washindi 100 wa TIME. Wanablogu wa Ki-Misri wana ya kueleza kuhusu jambo hili.
Azerbaijan: Bikra
Mwanablogu wa Emotions on Air, Mind Mute anatafakari marajio ya jamii kwamba wanawake watabakia mabikira mpaka watakapofunga ndoa. Japokuwa ipo nchini Azerbaijan, blogu hiyo inabaini mfumo unaofanana wa maadili katika...
Pakistani: Katika Vita
Mohammad Malick anatoa maoni juu ya shambulizi la kigaidi la hivi karibuni kwenye soko la watu wa tabaka chini na la kati huko Peshawar: “limeonyesha kuwa hii ni vita ambyo...