- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Syria: Mwanaharakati wa Haki Za Binaadamu Mwenye Umri wa Miaka 80 Akamatwa

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Syria, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Uhuru wa Kujieleza

Omar Mushawah ameripoti [1] [ar] kukamatwa kwa Haytham al-Maleh, mwanasheria wa Ki-Syria na mtetezi wa haki za binaadamu ambaye pia alitumia muda wa miaka 6 jela kati ya 1980 na 1986 kwa kudai mabadiliko ya kikatiba. Al-Maleh pia ni mwanzilishi mwenza wa Jumuiya ya Haki za Binaadamu ya Syria.