Malayasia: Serikali ya Jimbo Yaja na Sera ya ‘Msala Mmoja’

Waziri Mkuu wa Malaysia Najib Tun Razak ameanzisha wazo la Malaysia Moja, maarufu kama Malaysia1, alipoingia madarakani. Ikiwa ni nchi ya watu wa rangi tofauti, lengo kubwa la Malaysia1 ni kuukuza umoja wa kitaifa na kuimarisha ushirikiano baina ya makundi mbali mbali yenye rangi tofauti.

Sera ya Msala1 imeiga dhana ya Malaysia1

Sera ya Msala1 imeiga dhana ya Malaysia1

Kwa kuiga chapa ya Malaysia1, serikali ya Jimbo la Terengganu hivi majuzi ilikuja na sera ya ‘msala 1’ kama hatua kwa walimu na wanafunzi (wa jinsia moja) kuchangia misala (vyoo) ili kukuza hisia za umoja.

“Pale wanafunzi wanapochangia msala na mwalimu, wataamini (wanafunzi) kwamba wako sawa na wanataaluma na hii moja kwa moja huamsha hisia za kujichukulia kuwa na umuhimu katika taasisi, ambako, kwa mukhtadha huu, ni shule,” anasema mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Elimu ya Juu, Rasilimali watu, Sayansi na Teknolojia wa Jimbo hilo, Ahmad Razif Abd Rahman katika gazeti la mahali hapo la The Star.

Sera pia itapanuliwa zaidi ya suala la choo ambapo walimu pia wanashauriwa kula katika mikahawa ya shule pamoja na wanafunzi. Ni njia ya makundi hayo mawili (walimu na wanafunzi) kujichanganya wakati wa mapumziko.

Kumekuwa na maoni tofauti kutoka kwenye ulimwengu wa blogu kuhusiana na mada hii. Wengine waliichukulia kama utani, wakati wengine walifikiri ilikuwa ni ubunifu chanya.

Jeff Ooi, ambaye ni mwanablogu mkubwa na sasa ni Mbunge anasema:

Wakati huu, matunda ya kupanuka kwa Malaysia1 yako mahali pa kujisaidia.

Mwanablogu wa Life And Ti(m)es Of Liang Seng hakuweza kuamini kwamba Serikali ya Jimbo hilo inakuja na wazo la ‘Msala mmoja’:

Ningeelewa sehemu ya kuchangia mkahawa. Lakini hivi kweli kuchangia msala ni kukuza hisia za ushirikiano na kujenga mafanikio ya kitaaluma? Tuwe wakweli. Tunaweza kufanya vyema zaidi.

Mwandishi wa habari, mwanablogu na mwandishi wa Global Voices Niki Cheong anaandika kwenye blogu yake binafsi:

Kichaa yupi alikuja na wazo hili zuri […] Nadhani kuchangia msala na mwalimu hakutamsadia mwanafunzi kufanikiwa katika masomo yake, ufundishaji mzuri unaweza!

Ni nini kinachoendelea? Je, tunaenda kuanza kula ‘chakula kimoja’ baada ya hapa? Au kuanza kusikiliza ‘1 Buck Short’? Au tutaanza kuwataka watu kuandikisha majina kama ‘Sharina1’ kwenye vyeti vya kuzaliwa?

Mwanablogu wa Thots Here And There anaamini kwamba viongozi ni lazima watende wayasemayo kabla ya kutekeleza sera zozote:

Kwa nini tusianze na makundi ya tabaka la juu kwanza kabla kwenda kwa walio wengi? Shuleni kwangu, Kundi la tabaka juu hupata ufunguo maalumu kwa choo chao maalumu […] Najua kwenye makampuni fulani ya sekta binafsi kuna upendeleo wa namna hiyo pia. Nakumbuka rafiki yangu alipofurahi sana kwa sababu alikuwa amefikia kiwango cha upendeleo wa kuwa na ufunguo wake mwenyewe wa sehemu hiyo malum! Sasa, kama tunataka kutekeleza kitu kama hiki cha msala mmoja shuleni –fikiria wanafunzi watakavyopanga foleni kutumia msala –hebu na tuanze na kundi la juu la watumishi kwanza. Viongozi wanazungumza kuhusu Malaysia1 …tuwe wakweli, fanya usemacho. Tuonyesheni, enyi viongozi wa Malaysia kwamba sisi tu kitu kimoja kwa namna zote zinazoshirikisha matumizi ya msala!!!!

Mwanablogu wa Voices Inside My Head anaeleza upande chanya wa sera ya msala1:

Wakati nilipokuwa shuleni nilijiuliza jambo hili hili, inakuwaje walimu wajisaidie kwenye vyoo tofauti. Hivi wanajisaidia kwa namna tofauti? Hivi wana kitu kinginecho tusichokuwanacho sisi? Nadhani inatakiwa kufanyika pote, hata kwenye maeneo ya kazi ya utawala wa juu watumie vyoo hivyo hivyo! Labda hata mawaziri washirikiane vyoo na wafanyakazi wengine wa serikali na hapo ndipo nitakaposema wanasiasa wetu wanatenda wasemacho!

Mwandishi huyu, kupitia kwenye blogu yake binafsi, anasema:

Walimu pia wanapaswa kuongoza kwa mifano na kupata matokeo mazuri kwa wanafunzi wao. Kama mwanafunzi tayari ana tatizo la kujisikia duni awapo darasani, atawezaje kuibuka na hisia za kujiona wa maana kwa sera ya Msala1?

Hivi tunatakiwa kuchangia msala ili kuwa na hisia za umoja baina ya wanafunzi na walimu? Je, ushirikiano huu wapaswa kuanzia darasani kwenyewe?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.