- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Japan: Uchunguzi Mpya Juu ya Umaskini Waharibu Soga za Utajiri

Mada za Habari: Asia Mashariki, Japan, Mwitikio wa Kihisani, Uchumi na Biashara, Utawala

Mjapani mmoja kati ya sita anaishi katika umasikini inasema ripoti [1] mpya ya Wizara ya Ustawi wa Jamii [en]. Kwa mujibu wa takwimu [2]za OECD, Japan ina kiwango kikubwa zaidi cha umasikini katika dunia iliyoendelea na ni ya 4 baada tu ya Mexico, Uturuki na Marekani.

Na Flickr: Ushio Shugo

Na Flickr: Ushio Shugo

Mnamo mwezi wa Septemba, Makoto Yuasa, Katibu mkuu wa Mtandao wa Kupinga Umaskini [3] (反貧困 Han Hinkon) [ja], alilionyesha tatizo kwa kufafanua tatizo la umaskini nchini Japan kwa njia hii [4] [en]:

Tangu ukuaji mkubwa wa uchumi katika miaka ya 1960, Japan imerithi hadithi za ngano kuwa watu wote wa Japan wamo katika tabaka la kati (kiuchumi). Hata hivyo, mtindo wa ajira wa Kijapani, ambao upo katikati ya ngano hii, umebadilishwa kutokana na ongezeko la ajira holela na sababu nyingine, na idadi inayoongezeka ya Wajapani wanaishi katika umaskini.

Kama wengi wanavyojadili katika blogu zao, tofauti za mapato nchini Japan siku hizi si jambo jipya. Wakati futuzo la uchumi lilipopasuka mwanzoni mwa miaka ya 90 udhaifu uliopo kwenye mfumo wa Kijapani ulionekana na tangu hapo wataalamu wengi wanasema kuwa nchi haijapona kutoka kwenye hali mbaya ya uchumi.

Ysaki anaeleza [5] jinsi tatizo hili lilivyoendelea kuwepo na jinsi lilivyochukuliwa na Wajapani wengi kana kwamba ni tatizo la watu wengine.

この記事を最初に見た時に、私は部落問題に近いな、と感じたんです。それは、私たちの隣に確実にその問題があるのに、知らないふりをする。見ない振りをし、無関係を装ってきた。

Niliposoma habari nilihisi kuwa tatizo hili linafanana na lile la makundi mengine madogo nchini Japan.
Japokuwa kuna tatizo kwa hakika na lililo karibu sana nasi tunajidai hatulioni na kwa kufanya hivyo, tumeweza kujishawishi kuwa hilo si tatizo letu.

Miyabi-tale anachukulia kuwa suala hili lina historia ndefu na kwamba lawama ni lazima zirudishwe kwenye kushindwa kutoa maamuzi kwa wanasiasa.

驚くべきは、この数字が今年ではなくて数年前のデータでさえすでに7人に1人いるという事実で、リーマンショック以降の世界恐慌の不景気のあとでは今現在では少なく見ても5人に1人はそれくらいの値になっていると考えられることである。自民政権下では、公式発表的に「日本に貧困はない」「一億総中流家庭」なんていうキャッチコピーもあったわけだが、現実はまったくそうでないということが改めて浮き彫りにされたわけである。

Jambo linashongaza ni kuwa takwimu zilizotolewa miaka michache iliyopita zilionyesha kuwa mmoja kati ya watu saba anaishi katika umaskini. Kuna wengine wanaoliona hili kuwa ni chanya yaani, licha ya hali mbaya ya uchumi iliyoathiri dunia nzima baada ya kuanguka kwa Lehman Brothers, siku hizi ni mmoja tu kati ya watu watano ni maskini.
Chini ya serikali ya LDP, kauli mbiu kama vile ‘Katika Japan Hakuna Umaskini’ au ‘Jumla ya kaya za tabaka la kati mia moja milioni’ zilikuwa zikitangazwa lakini imekuwa dhahiri tena kwamba hayo yalikuwa mbali na ukweli.
Na Flickr: Caribb

Na Flickr: Caribb

Kuna wengine hata vivyo ambao wanapendelea kuangalia upande mwingine wa sarafu.
Ukkii anatumaini [6] kwamba kipindi hiki cheusi katika historia ya kijamii na kiuchumi ya Wajapani kitarejesha ngvu za kiroho ambazo watu wa Japani wanajulikana kuwa nazo.

し・か・し
国の景気が良くなるまでこのままでいいのだろうか
貧しかった戦後の日本国民は、みな必死で頑張ってここまでよくなってきています
あの時代のハングリー精神があればきっと国を変えれなくとも企業の生き残りは可能だと思います
私は一社員でありますが社長のような視点で物事を考えていくことを目標としています
視野を広げればいろんなことに発見や改善が見えてくるからです
ハングリー精神なんて言葉、現代では死語なのかもしれませんが
僕はこの言葉を提唱していきたいと思います

LAKINI
Je ni sawa kwa mambo kuendelea hivi mpaka uchumi wa nchi utakapoimarika?
Wakati watu wa Japan walipokuwa maskini baada ya vita, walifanya walichoweza bila kusita na wakaweza kuboresha hali kama tunavyojua leo.
Ikiwa tu tutakuwa tena na ROHO YENYE HAMU ya wakati ule nina hakika kuwa hata kama hatuwezi kuibadilisha nchi yote mara moja, kuzifanya kampuni zetu ziwe imara na zinazoweza kushindana hilo linawezekana.
Mimi ni mwajiriwa lakini ninajaribu kuangalia mambo kutoka katika mtazamo wa Mkurugenzi Mtendaji kwa sababu ikiwa tuna uwezo wa kuona mbali, kuna ugunduzi mwingi na uboreshaji unaoweza kufanyika, ambao unaweza kutumika katika mambo mbalimbali.
Neno ‘roho yenye hamu’ pengine limesahaulika siku hizi lakini ningependa kuliweka mbele tena.