Cambodia: Tuzo yamuenzi aliyenusurika na utumwa wa ngono

Sina Vann alikuwa na umri wa miaka 13 wakati alikupoja Cambodia kutoka Vietnam kwa kile kilichopaswa kuwa likizo. Badala yake, aliuzwa kama mtumwa kwa ajili ya ngono na alitumia miaka miwili iliyofuata ndani ya danguro. Alikombolewa wakati Somaly Mam, mwanaharakati wa kupinga utumwa na sura ya Taasisi ya Somaly Mam, alipopanga uvamizi kwenye danguro alilokuwa akiishi Vann. Leo, Vann ni mwanaharakati wa Taasisi ya Somaly Mam, akiwasaidia wanusurika wengine wa utumwa huo pamoja na wale wanaoendelea kutaabika kwenye madanguro.

Kwa kazi aliyofanya Vann, alituzwa tuzo ya Frederick Douglass. Tuzo ya Frederick Douglass “huenzi uwezo wa kumudu wa roho ya binadamu na husisitiza kwamba wengi wa wanaonusurika utumwa wa ki-leo huendelea kuwasaidia na wengine kuwa huru”

Habari zaidi kuhusu Vann zimeonyeshwa kwenye video hii:

2009 Frederick Douglass Award Winner – Sina Vann from Free the Slaves on Vimeo.

Mshindi wa tuzo ya mwaka 2009 ya Frederick Douglass – Sina Vann kutoka Free the Slaves katika Vimeo.

Hivi karibuni, Umoja wa Mataifa uliongeza mwaka mmoja zaidi wa mamlaka yake kushughulikia hali ya haki za binadamu nchini Cambodia. Kwa mujibu wa gazeti la The Mirror, mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa, akitoa taarifa kwenye Baraza la Haki za Binadamu:

Alionyesha kuguswa na hali ya haki za binadamu nchini Cambodia. Kwa mujibu wa taarifa yake, utawala wa sheria nchini Cambodia ni dhaifu…Pia, alitaja suala la Mbunge wa Chama cha Sam Rainsy –kutoka kwenye chama kikuu cha upinzani nchini Cambodia – Bi. Mu Sochua, aliyehukumiwa na mahakama, kwa shinikizo la serikali ya Chama tawala cha CPP, kupoteza kesi hiyo katika mazingira yasiyo ya haki, kwa sababu alithubutu kupinga dhidi ya wenye nguvu nchini Cambodia.

Wengine walimsihi Mwakilishi huyo Maalum asiwasahau wanawake na watoto ambao bado ni wahanga wa utumwa wa ngono nchini Cambodia, kwa kuzingatia kwamba hilo ni lazima libaki kuwa kipaumbele cha haki za binadamu kwa sababu uvunjifu wa haki nyingine za binadamu, mfano uhuru wa kujieleza, unaendelea kushika kasi.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.