Habari kutoka 27 Oktoba 2009
Uchaguzi Tunisia: haki Bila Ya Upendeleo!!?
Rais wa Tunisia Zine Al Abidine Ben Ali ameshinda uchaguzi kwa kipindi cha tano kwa asilimia 89.62 ya kura zote. Chama chake cha Democratic Constitutional Rally kilishinda viti vya bunge 161 katika viti 214. Wanablogu wa Tunisia wanatoa maoni katika makala hii.
Malayasia: Serikali ya Jimbo Yaja na Sera ya ‘Msala Mmoja’
Kwa kuiga chapa ya Malaysia1, serikali ya Jimbo la Terengganu hivi majuzi ilikuja na sera ya ‘msala 1’ kama hatua kwa walimu na wanafunzi (wa jinsia moja) kuchangia misala (vyoo) ili kukuza hisia za umoja. Kumekuwepo na maoni mchanganyiko katika ulimwengu wa blogu kuhusiana na sera hii.