Philippines:Mafuriko Mabaya Zaidi Katika Kipindi cha Miaka 40

Zaidi ya watu 50 wamefariki baada ya kimbunga kilichopewa jina la “Ondoy” (Jina la Kimataifa: Ketsana) kilipolipiga jiji la Manila na majimbo jirani. Kimbunga hicho kilisababisha mafuriko mabaya zaidi nchini katika kipindi cha miaka 40 na kuwapotezea makazi watu 280,000 jijini Manila na katika majimbo mengine , kuna watu zaidi ya 41,000 kwenye vituo vya dharura. Wakati makala hii inaandikwa, wakazi milioni 1.2 bado hawana umeme katika mji mkuu wa Philippines.

Tovuti za kijamii zilitumika vyema siyo tu kwa kupashana habari zinazohusu mvua hiyo kubwa bali pia kuripoti jitihada na kesi za dharura kwenye sehemu zilizoathika na janga hilo. Joey Alarilla anaangalia jinsi intaneti ilivyotumiwa na wanamtandao wa Kifilipino wakati kumbunga kilipoikumba Manila.

Ninablogu kwa kutumia modemu ya HSDPA USB kwa sababu makazi yetu bado hayana umeme baada ya masaa kadhaa, na bado nina bahati zaidi kuliko wengi wa wananchi wenzangu, ambao baadhi bado wamekwama njiani au bado wako kwenye mapaa ya nyumba zao

Twita na mitandao mingine ya kijamii kama vile Facebook ndiyo njia pekee ambazo watumiaji wa intaneti wa Kifilipino wamekuwa wakizitumia kwenda sambamba na maendeleo pamoja na habari nyingine kama vile kutuma namba za mashirika ya misaada ya dharura na mashirika ya kujitolea hasa hivi sasa wakati mitandao ya simu imefurika.


Kituo cha Taarifa za Uokoaji kina lahajedwali ambayo ina orodha ya watu walioathirika na mafuriko ambao wanahitaji kuokolewa. Ramani ya google pia ilitengenezwa ili kufuatilia maeneo yaliyofurika katikati ya jiji la Manila na kuongoza mamlaka kwenye vijiji ambako waathirika na mafuriko wanahitaji msaada.

Angalia ramani kubwa ya hali ilivyo katika Kimbunga cha Ondoy katikati ya jiji la Manila

Wafilipino pia walitumia Twita na Plurk kufuatilia habari za kimbunga kadiri zilivyokuwa zinatokea, kwa kweli, “Ondoy” na “NDCC” (Baraza la Taifa la Kuratibu Majanga) viliondokea kuwa mada maarufu zaidi kwenye Twitter Jumamosi iliyopita. Hii ni mifano ya jumbe za Twita:

pretzelgurl: baba yangu bado amekwama kazini kwake huko manggahan, mjini pasig. tafadhalini tumeni msaada
angeliesa: Aliruhusiwa na profesa majira ya mchana. Alitembea na kuhangaika kwenye mafuriko. Alifika nyumbani majira ya saa 2 usiku. Hivi sasa mwili wangu wote u dhaifu
janblando: Bibi yangu bado amekwama kwenye kibanda chake cha kienyeji, huko Cainta. Mafuriko mtaani kwake ni kima cha kiuno na mkondo wake una nguvu.
ValfrieClaisse: Oh mie! Hakuna umeme hapa tangu jana. Mafuriko makubwa na machafu yameivamia jamii yote.
dementia: kuna misaada mingi inayoingia lakini kinachotakiwa ni njia ya kusafirisha vifaa kwa waathirika
teeemeee: mafuriko yameshuka chini katika eneo letu la kuegesha magari lakini bado bado ni kima cha magoti au kiuno. Kina kilifikia Karibu na kifua jana usiku
ArmelEspiritu: Ndio kwanza nimefika nyumbani baada ya kukesha kwenye gari langu. Ilinibidi nilipeleke sehemu ambyo hakuna mafuriko ili kulinusuru

Kuna filamu kadhaa za video zilizopandishwa kwenye Youtube ambazo zinaonyesha madhara ya mafuriko katikati ya jiji la Manila. Video ya kwanza: mafurikokatika mji wa Makati, kitovu cha biashara nchini. Video hii ilipakiwa na yugaabe

Video hii inaonyesha mafuriko katika mto Marikina. Video ilipakiwa na Initiate360

Katika mtaa wa Katipunan, basi dogo lilizama kwenye barabara iliyofunikwa na maji.

Waendao kwa miguu wakijaribu kuvuka barabara iliyofurika

Michango bado inahitajika. Kuna vikundi kadhaa ambavyo bado vinapokea michango kwa ajili ya walioathirika na mafuriko.

Picha kutoka kwenye Ukurasa wa Flickr wa rembcc

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.