Marekani: Stempu ya Iddi Yachochea Chuki Huko Tennessee

Toleo la stempu la mwaka 2008, kabla bei haijapanda

Toleo la stempu la mwaka 2008, kabla bei haijapanda


Wakati Waislamu nchini Marekani wanasherehekea Eid al-Fitr, sherehe inayoadhimisha mwisho wa mwezi wa Ramadhani, barua pepe yenye nia mbaya imekuwa ikizunguka. Barua pepe hiyo ina maddai ya uongo kuwa Rais Obama ametoa stempu mpya kuadhimisha sherehe mbili za Eid na kuwataka wasomaji wa barua pepe hiyo kuigomea hiyo stempu, huku ikiorodhesha mashambulizi ya kigaidi yalifonywa nchini Marekani katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita. Maandishi ya hiyo barua pepe yanaonekana kwenye makala hii ya Missives from Marx, ambaye anaelezea kughafirika kwake kulikotokana na barua hiyo:

Nilipokea barua pepe ifuatayo leo kutoka kutoka kwa ndugu yangu. Kutokana na mambo kama haya ndiyo maana nitazitumia wiki nne za mafunzo yangu ya dini (Western Religious Course) kuzisambaratisha imani potofu juu ya Uislamu. Ndio maana uchambuzi yakinifu ni lazima uwe sehemu muhimu ya masomo yangu.

Na kama ilivyoondokea, hakuna jipya kuhusu hii barua, au stempu. About.com inafafanua kuwa barua hii imekuwepo tangu mwaka 2002, wakati stempu yenyewe ilitolewa tarehe 1, Septemba 2001.

Aziz Poonwalla, katika blogu ya City of Brass kwenye BeliefNet anafafanua habari ya hii barua pepe:

Matoleo ya hiyo barua pepe, ambayo yamekuwa yakizungushwa kwa miaka kadhaa, yameshachambuliwa lakini bado yanaendelea kusambazwa. Nimeblogu kwa kirefu kuhusu historia ya stempu hiyo ya Eid, utata uliombatana nayo wakati ilipotolewa (hasa kutoka kwa wahafidhina wa chama cha Republicans), na utetezi wa stempu hiyo uliofanywa na Rais Bush pamoja na Spika Hastert. Kwa kifupi, stempu hiyo ilitolewa tarehe 1 Septemba 2001, siku kumi kabla ya mashambulizi ya 9-11, wakati wa serikali ya Bush. Meya Piper anajiunga na orodha ndefu ya wanasiasa wahafidhina ambao hawana pingamizi na stempu zinazoadhimisha sikukuu za Hanukkah, Kwanzaa, na hata mwaka mpya wa Kichina – bali stempu iliyotolewa kwa ajili ya sikukuu ya Kiislamu ya Eid imetengwa kama tishio, na kuwataka Wamarekani wazalendo waiwajibikie?

Makala kwenye Clarksville Online, blogu ya mji wa Clarkstown, Tennessee, inaelezea ni kwa nini hii barua pepe imesababisha vichwa vikubwa vya habari mwaka huu:

Meya wa Clarksville Tennessee, Johnny Piper ametuma barua pepe ya kichochezi inayopinga Uislamun kwa wafanyakazi wa mji huo, inayowaasa waisusie hiyo stempu iliyotolewa na husduma ya posta ya Marekani…

… Meya Piper anajaribu kutetea vitendo yake, lakini vitendo hivyo ni vigumu kutetewa. Waislamu ni sehemu mojawapo ya nchi hii. Wanatumikia kiadilifu kwenye majeshi yetu ya ulinzi, wanalilinda taifa, na uhuru wetu. Hakuna mtu nayepaswa kuchukuliwa kama raia wa tabaka la pili kwa misingi ya imani yake ya kidini, au kutokana na vitendo vya watu wenye siasa kali wachache. Tukio hili lililotengenezwa na Meya wetu limekuwa ni aibu kwa mji wetu, jimbo, na nchi yetu.

Sheila Musaji amekuwa akifuatilia mzunguko wa barua pepe hiyo inayohusu stempu kwa ajili ya jarida la The American Muslim (TAM) tangu mwaka 2005, na katika moja ya habari zake, anatoa maoni juu ya vitendo vichafu vya Meya Piper:

Nina hakika kuwa Meya wetu mzuri alishangazwa na ghafla ya iftar iliyofanywa na Obama kwenye Ikulu ya Marekani.

Na, kama ilivyo kawaida maneno ya mwisho ya wabaguzi wote huwa: ‘nina marafiki kasha wa Kiislamu,” aliongeza.”

Pengine marafiki hao wazuri wa Kiislamu wanaweza kumuelimisha ni kwa nini makala HII (PDF) inagadhabisha.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.