- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Korea: Ziara ya Clinton Korea Kaskazini

Mada za Habari: Asia Mashariki, Korea Kusini, Habari za Hivi Punde, Mahusiano ya Kimataifa, Siasa, Vita na Migogoro

Habari ya kushangaza. Kwa ghafla, Clinton alizuru Korea ya Kaskazini na kama vile 007 aliwarudisha nyumbani wanahabari wawili wa kike ambao walikuwa wameshikiliwa nchini Korea Kaskazini. Kuhusiana na habari hii ya ghafla, hakuna habari zilizowekwa kwenye vyombo vya habari vya umma vya Korea na hata kwenye maoni ya wanablogu. Zifuatazo ni makala chache.

1: [1]

Rais wa Zamani wa Marekani Clinton alizuru Korea Kaskazini kwa ghafla na kuishangaza dunia nzima. Pengine Marekani ilikuwa na hii karata tayari katika mikono yake, lakini ilitumia karata nyingine. Kwa ghafla, Korea ambayo ilikuwa ikisisitiza ‘hatua dhabiti za kukabiliana’ iligeuka. Kwa hiyo, Korea Kaskazini itasisitizia zaidi ‘mazungumzo na Marekani pamoja na kuizuia Korea ya Kusini’ na hivyo mazungumzo baina ya Korea Kaskazini na Marekani yataweza kuanza.
Japokuwa ilikuwa ni ziara binafsi, Clinton ni rais wa zamani wa Marekani, na mkewe ni katibu wa sasa wa mambo ya nje. Kwa hiyo ni sawa tu na mazungumzo ya kiserikali. Ni wazi, kuwa kulikuwa na uharaka wa kuwaokoa ‘mateka’ wale wawili na kuwarudusha Marekani. Wakati Hilary alipotaka ‘warejeshwe’, mchakato ungeliweza kuanza. Alitaka ‘warejeshwe’ tofauti na kutaka ‘waachiwe mara moja’ kama sharti la kulitazama upya suala Korea.

Pengine muda wa kuuliza ni kwa jinsi gani Clinton aliweza kuzuru Korea Kaskazini umepita. Nadhani (ziara hiyo) ilikuwa imepangwa kwa kitambo. Ni mbinu ya kidiplomasia ambayo chama cha Demokrati imetumia katika utamaduni wake. Carter alizuru Korea Kaskazini baada ya mgogoro wa Silaha za Nyuklia wa mwaka 1994 na Madeleine Albrigyt pia alizuru Korea Kaskazini mwaka 2000. Dhahiri, mahusiano baina ya Korea Kaskazini na Marekani yaliboreshwa. Lakini baada ya Bush hali imebadilika sana. Japokuwa chama cha Demokrati kilitawala, hali imekuwa mbaya kutokana na hali ya kisiasa ya Korea Kusini. […]

Kabla ya mlolongo wa matukio haya, tulikuwa na fursa kadhaa za kutatua matatizo haya sisi wenyewe. Lkakini kutokana na sera kidiplomasia sizizojali za serikali mpya mafanikio yote ambayo tuliyapata yamegeuka sifuri na tumejikuta katika hali ya mgogoro. Sijui ni nini tulichopata, lakini jambo moja lipo wazi. Kuanzia sasa na kuendelea, nina hakika kuwa hatuna uwezo wa kufanya majadiliano ya amani ya kupunguza silaha. Tutakuwa tunaburuzwa na Korea kaskazini pamoja na Marekani. […]

2: [2]

Ili kuwaokoa watu wao, rais wa zamani hakusita kwenda kwenye makao ya adui. Lakini ni nini serikali yetu ilichofanya? Kwa kupitia njia za ain azote za kidiplomasia, walifanya juhudi za kuwaokoa salama. Lakini je serikali yetu inafahamu kuwa Bw. Yoo na mabaharia wa meli ya Yeonan wapo hai au ni dhiki kiasi gani inayowakabili sasa? Ikilenga jumuiya ya kimataifa, Korea Kaskazini mar azote hutumia mbinu za kutisha, lakini serikali (yetu) huangalia tu huku imekunja mikono. Na kwa kuongeza, tunapaswa kuikemea vikali Korea kaskazini kwa kukiuka haki za binaadamu bila ya sababu zozote. Serkali isimuangalie tu rais wa zamani Clinton na ibadilkishe mtazamo wetu kwa vitendo. Pia inatupasa tufikirie kufunga kanda ya viwanda ya Kaesong kama uhusiano wetu hautaboreshwa.

3: [3]

[…] Nilipotazama habari asubuhi hii, nilisisimka. Clinton alikwenda Pyongyang peke yake. Nilitumaini hie hivyo wakati wa utawala wake. Nilitumaini hili lingefanyika wakati wa utawala wa Bush. Nilifikiri baada ya Obama uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Marekani ungekuwa tofauti, lakini hilo halijatokea bado. Mgogoro wa vita katika bahari ya Magharibi unapelekea kuwa mgumu zaidi na waltu wanaofanya kazi katika taasisi za muungano wako jela. Katika hali hii ya kukata tama, mara Clinton alizuru Korea Kaskazini.

Ningependa kumshukuru Clinton kwanza. Sikufurahia kuhusu mke wake ambaye kila mara huiongelea vibaya korea kaskazini. Baada ya simulizi kadhaa, hatimaye aliwasili mjini Pyongyang na ninamshukuru kwa hilo. Natumaini atawachukua wanahabari wale wa kike na pia atavichukua vita baridi pamoja naye. Natumaini atachukua pia migawanyiko. Inaonekana kuwa serikali ya Korea ilifahamu juu ya ziara ya Clinton. Na katika siku hiyo hiyo, wanateketeza Kiwanda cha magari cha Ssangyong. Inanuka. […] Nasikia kuwa atarejea keshi. Anga mjini Seoul lina mawingu na kuna joto. Natumaini kuwa anga la Pyongyang ni angavu. Natazamia mvua, mvua ya amani na mvua ya muungano…