19 Julai 2009

Habari kutoka 19 Julai 2009

Afrika Kusini: Kuvuvuzela au Kutovuvuzela?

Mjadala kuhusu kifaa maarufu kinachoitwa vuvuzela kinachopigwa na mashabiki wa mpira wa miguu Afrika Kusini umetawala katika blogu mbalimbali duniani tangu kuanza kwa Kombe la Mabara la mwaka huu nchini Afrika Kusini, lililohitimika wiki iliyopita. Waandishi wa habari, watazamaji wa televisheni, makocha na baadhi ya wachezaji wa kigeni walitoa wito wa kusitisha matumizi ya kifaa hiki katika Kombe la Dunia la 2010 nchini Afrika Kusini. Mabishano haya yana sauti kubwa kama chombo chenyewe.