- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Ramani ya Ulimwengu wa Blogu za Irani Siku ya Mkesha wa Uchaguzi

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Iran, Harakati za Mtandaoni, Siasa, Teknolojia, Uchaguzi

John Kelly na Bruce Etling wanaelezea utafiti wao unaohusu ulimwengu wa blogu za Irani na uchaguzi katika blogu ya Intaneti na Demokrasi [1]. Intaneti na Demokrasi ni blogu ya timu ya mradi wa Intaneti na Demokrasi wa Kituo cha Berkman cha Intaneti & Jamii kilichoko Harvard.

Kufuatana na ufuatiliaji wetu wa ulimwengu wa blogu za Irani siku ya mkesha wa uchaguzi, inaonekana kuwa Mousavi anaungwa mkono na watu wengi kwenye mtandao wa intaneti kuliko Amhadinejad. (Ili kuelewa kwa mapana makundi tofauti nchini Irani angalia ramani yetu mpya shirikishi ya Ulimwengu wa blogu za Irani [2]). Ramani hizo zinaonyesha ni nani anayejiunganisha na tovuti zinazohusiana na wagombea. Inavutia kuona tofauti kati ya ahmadinejad (emtedadmehr.com [3]), ambaye ana viunganishi vingi kwenye kundi la siassa za kihafidhina, na Mousavi (mirhussein.com [4]) ambaye viunganishi vyake vinatokea kwenye sehemu zote za ramani, siyo tu kutoka kwenye kundi la mageuzi.


Tunashangazwa na viunganishi vinavyotokea kwenye kundi la washairi, ambalo ni kwa nadra sana hujiunganisha na tovuti za siasa. Kadhalika, Mousavi ana viunganishi vingi vinavyotokea kwenye kundi la mtandao wa madhehebu ya Shia kuliko Ahmadinejad.

Siyo lazima kuwa mvuto huu wa kwenye mtandao wa intaneti unaenda sambamba na duniua iliyo nje ya mtandao huo, bali unaweza kuashiria jinsi Mousavi alivyoongeza shamrashamra kwa wapiga kura, hasa kati ya wale ambao wako nje ya kundi linalotarajiwa kumuunga mkono, hali ambayo itasababisha watu wengi kujitokeza kumpigia kura Mousavi.

Kama vile Hamid Tehrani alivyoandika [5] mapema wiki hii, zana ya YouTube inatumiwa vilivyo na Wairani wengi katika uchaguzi huu. Ifuatayo ni filamu moja ya YouTube ambayo imunganishwa na wanamageuzi wengi.

Na hii ni video iliyounganishwa na wahafidhina wengi, ambayo hamid aliilezea mapema wiki hii kuwa ni mfano wa mmoja wa wahifidhina wanaoutumia kumdhihaki Khatami, ambaye anamuunga mkono Mousavi tangu pale yeye binafsi alipojitoa kwenye kinyang’anyiro.

Wataalamu wa mambo ya Irani wanatahadharisha dhidi ya kubashiri washindi wa uchaguzi nchini Irani (kwa sababu tumewahi kushangazwa huko nyuma), na tunapenda kutahadharisha kubashiri ushindi wa Mousavi kutokana tu na upembuzi huu, hata hivyo ni jambo linalovutia kuona Mousavi anaungwa mkono kiasi hiki kwenye mtandao wa intaneti siku ya mkesha wa uchaguzi. Inatubidi tuwaachie hilo wapiga kura.

Takwimu nyingine na upembuzi kuhusu mkesha wa uchaguzi wa Irani katika ulimwengu wa blogu vipo kwenye blogu ya Morningside Analytics Shifting the Debate [6]. Pia unaweza kuangalia mahojiano na kusoma makala zote za Hamid Tehrani [7] kwenye mtandao wa Intaneti na uchaguzi wa Irani kwenye tovuti ya PBS. Angalia tena sehemu hii wiki ijayo ili uone toleo letu la ulimwengu wa blogu za Kiarabu na matukio yanayombana katika USIP.