Gumzo la moja kwa moja kuhusu Virusi vya ukimwi na Ukimwi mtandaoni Tarehe 6 machi


Mradi wa Rising Voices na Global Voices wanaandaa gumzo la moja kwa moja mtandaoni kwa wanablogu na wanaharakati siku ya Ijumaa mwezi wa tatu mwaka huu(saa 11 jioni kwa saa za Nairobi) mada kuu ikiwa jinsi ya kublogu na kuongeza uelewa na habari kuhusu virusi vya ukimwi na Ukimwi.

Kila mmoja anakaribishwa

Muda:New York 3 asubuhi | Buenos Aires 6mchana | London 8mchana | Johannesburg,Beirut 10jioni | Nairobi, Moscow 11 jioni | New Delhi 1:30 usiku | Hong Kong 4usiku | Tokyo 5 usiku

Chumba cha gumzo:http://www.worknets.org/chat/

Jinsi ya kujiunga:Bonyeza kingo hapo juu tumia jina lako.Kisha chagua chumba utakacho kujiunga kwa kubonyeza ingia.Baada ya kuingia chagua ukubwa wa maandishi upande wa kushoto wa kiwambo cha tarakishi yako, jiunge katika gumzo

Gumzo la tarehe 6 mwezi wa 3 litajenga mada iliyoletwa katika majadiliano yaliofanikiwa wiki iliyopita. Gumzo la tarehe 27 mwezi wa pili lilitoa tamko kama vile umuhimu wa kublogu kwa watu walioathirika na virusi vya ukimwi na jukumu katika upelekaji na ushawishi wa maarifa,lakini kikubwa lililenga kwenye muongozo wa kublogu vyema ,muongozo ulitengenezwa na Global Voices kutoa ushauri tunu jinsi ya kublogu kuhusu masuala ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi. Muongozo huo bado ni kazi inayooendelea, kwa hiyo tunatafuta msaada kutengeneza na kutoa matokeo. Kwa wale waliokuwa na nia au waliokwisha blogu kuhusu maafa wanahimizwa kushiriki katika gumzo wiki hii, hasa wale wanaoishi au walioathirika na virusi vya ukimwi. Gumzo la Ijumaa litalenga masuala kama vile uanzishwaji makundi maalum ya kazi au vitengo kwa ajili ya mchakato wa kutengeneza muongozo wa kublogu vyema kadhalika gumzo hilo litajadili kuhusu aya na na mada zipi zijumuishwe kwenye muongozo.

Pia kuna mada nyingine ambazo utataka kujadili wakati wa gumzo,tafadhali weka maoni chini.Natumaini mtashirikiana nasi tarehe 6 mwezi wa tatu

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.