Ukraine: Umaarufu wa Yushchenko Unafifia

Kwa mujibu wa kura ya maoni iliyofanyika mwezi uliopita, Rais wa Ukraine Victor Yushchenko “angeshinda chini ya asilimia 2.9 ya kura kama uchaguzi wa rais ungefanywa mwishoni mwa mwezi desemba 2008 au mwanzoni mwa mwezi wa Januari 2009.” Kati ya sababu za matokeo hafifu ya kura ya maoni ni “migogoro ya ndani isiyoisha” kati ya rais na Mwaziri mkuu Yulia Tymoshenko.

Tarehe 5 Februari, baraza la mawaziri la Tymoshenko lilinusurika kuondolewa baada ya kura ya kutokowa na imani katika bunge: waliopendekeza kura hiyo walishinda kwa kura 203 katika bunge la viti 450; kura 226 zinahitajika ili muswada upite. Levko wa Foreign Notes aliandika haya kuhusu matarajio ya kura hizo kwa rais na maswahiba wake wa kisiasa:

Manaibu wajumbe [NUNS] 10 tu ndio waliounga mkono muswada wa kutokuwa na imani uliofadhiliwa na [PoR] katika serikali inayoongozwa na Tymoshenko katika bunge la Ukraine leo hii. Miongoni mwa wajumbe hao 10 lilikuwepo kundi la ‘Yedyniy Tsentr’ linaloongozwa na mkuu wa sekretarieti ya rais Viktor Baloha pamoja na kaka yake Yuschenko, Petro.

Idadi hiyo ni habari mbaya kwa rais. Wajumbe wanaomuunga mkono rais waliingia bungeni wakiwa na manaibu 72 wakati wa majira ya kipupwe 2007. Wakiwa wanazidi kupungukiwa na msingi wa nguvu, nafasi ya Yuschenko kushika awamu ya pili ya urais inakaribia na kutokuwepo. […]

Kadhalika tarehe 5 Februari, mtumiaji wa LJ, kotyhoroshko aliandika hivi [UKR] kuhusu rais:

Njia ya nchi kujinusuru

Hivi sasa Yuschenko ana wasaa muafaka wa kujiuzulu.

Kujiuzulu kwake kutaleta ufumbuzi kwa kiasi Fulani kwenye mgogoro wa kisiasa.

Pia ataepuka matatizo yasiyo ya lazima yanayohusiana na kampeni ya uchaguzi [wa raisi unaokaribia].

Hatazama kwenye [masuala ya kupinga habari zinazomhusu].

Pengine, miaka 20 ijayo, hatakumbukwa kama rais mbaya zaidi. Kumbukumbu za watu ni fupi.

Yafuatayo ni baadhi ya maoni kwenye makala hii (UKR):

marmuletka:
Kwa bahati mbaya, Yuschenko hasomi blogu yako LJ.

***
ukrainietis:
Atatukuzwa tena si katika miaka 20 ijayo bali katika miaka miwili au mitatu ijayo. Kwa sababu wale watakaochukua nafasi yake inawezekana kabisa kuwa [hawana uwezo]

***

gonchar73:
Tatizo ni kwamba muhimili wa Yuschenko umejaa wale wanaofaidika na kuwepo kwao Karibu na rais. Ndio hao wanaomkaba koo, wakiimba na kumpa hakika na mapovu vinywani mwao kwamba bado hajamaliza kazi yake. Na hii ndio sababu wanaomzunguka Yuschenko hawataruhusu hili litokee. Lakini naafiki – ni wakati mzuri mno japo akikiri hivi: “sitagombea muhula mwingine na sitaweka vipingamizi kwa serikali mpaka mwisho wa muhula huu. Na kuanzia sasa, uwajibikaji wa kitaifa uko kwenye mikono ya serikali.

***

irishhighlander:
Uamuzi mzuri zaidi ni huu: waache wale ambao wana vipaji visivyotambulika kitamaduni kwa pamoja waongoze nchi. Halafu uondoke. Wote – Yuschenko na Tymoshenko, na [Yanukovych], na bunge lote. Na vizuri zaidi – jumuiya nzima ya hara-kiri.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.