Habari kutoka 26 Oktoba 2008
Bahrain: Raha na Karaha za Kusoma Ng'ambo
Ingawa Bahrain ina idadi kadhaa ya vyuo vikuu, vya umma na binafsi, raia wengi wa nchi hiyo hupata fursa ya kwenda ng'ambo kwa masomo ya shahada ya kwanza na hata zile za juu, mara nyingi kwa kutegemea ufadhili. Moja ya matatizo ya kwanza wanayokumbana nayo huko ughaibuni ni kwamba watu wachache tu hufahamu ni wapi Bahrain ilipo. Katika makala hii tunafuatilia uzoefu wa wanablogu watatu ambao ndiyo kwanza wamekwenda ng'ambo kwa masomo: kule Japan, Uingereza na Marekani na mwanablogu wa nne ambaye anasoma India kwa kipindi fulani hivi sasa.
Misri: Sisi sote ni Laila
Sisi sote ni Laila, ndivyo wanavyosikika kusema kwa sauti moja wanablogu wa kike wa Misri. Hivi, huyu Laila ni nani na kwa nini wasichana na wanawake wa kiMisri wanapenda kufananishwa naye? Hebu endelea kusoma ili uone ni kwa namna gani wanablogu wa Misri wanavyojihangaisha ili kuvunjilia mbali vikwazo vya jinsia na kufanya sauti zao zisikike.
Afrika ya Kusini: VVU na UKIMWI na mabadiliko ya sera
Mwishoni mwa mwezi Septemba, Barbara Hogan, aliteuliwa na Rais wa mpito Kgalema Motlanthe kuwa waziri mpya wa afya wa Afrika ya Kusini, akichukua nafasi ya mtangulizi wake mwenye utata mwingi, Manto Tshabalala-Msimang. Wanaharakati wa masuala ya UKIMWI na raia wengi wa Afrika ya Kusini wana matumaini makubwa kwamba hatua hii...