- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Angola: Uchaguzi Katika Picha

Mada za Habari: Popular Post, One month, First Post!, Two Posts, Three months, Five Posts, Six months, Ten Posts, One year, Two years, Twenty-five Posts, Fifty Posts, Five years, Seventy-five Posts, One Hundred Posts, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Angola, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi

Ijumaa hii ya tarehe 5 Septemba ilikuwa ni siku maalum katika Angola. Baada ya kampeni vuguvugu za uchaguzi [1], umma ulijawa shauku ya kupiga kura [2]kwa ajili ya bunge jipya baada ya miaka 16. Kwa watu wengi, hii ilikuwa ni fursa yao ya kwanza kutumia haki yao ya kupiga kura. Wengi wa watu hao walikwenda kwa amani [3] kwenye vituo vipatavyo 12, 000 vya kupigia kura, ingawa upigaji kura huo utaendelea katika vituo 320 vilivyoko Luanda kutokana na matatizo ya kimipango yaliyosababisha uchelevu wa makasha ya kura jijini humo.

Wakati ambapo maoni yanaanza kujitokeza katika mtandao wa wanablogu, ripoti kamili iko njiani.Kwa sasa zifuatazo ni picha [4]zinazoonyesha siku hiyo ya kihistoria, kama zinavyoorodheshwa na Jose Manuel Lima da Silva, mtumiaji wa huduma ya Flickr Kool2bBop [5], pamoja na nukuu zake:

Umoja wa Kitaifa. Angola inuonyesha ulimwengu kwamba, pamoja na tofauti zilizopo, ina wananchi wenye mshikamano. Watu wamoja na Taifa moja. Tunatumaini kuwa itakuwa hivi mpaka mwisho – moyo wa kitaifa!

Kuna picha nyingi zaidi za siku hiyo kubwa kwenye tovuti za picha za Flickr za Tiago Sousa [6]na Sam. Seyffert. [7]

Karibia watu milioni 8.3 wamejiandikisha kupiga kura, ili kuchagua wagombea zaidi ya 5,000 kutoka katika vyama 10 vya siasa na vile vya mseto. Kuna jumla ya viti 220 vya bunge.