Habari kutoka 22 Septemba 2008
Angola: MPLA Yashinda Zaidi Ya Asilimia 80 Ya Kura na Kutwaa Viti 191
Tume ya taifa ya Uchaguzi nchini Angola imetoa matokeo ya mwisho ya Uchaguzi wa kwanza wa kitaifa katika miaka 16 na imethibitisha ushindi wa chama tawala, Chama Maarufu kwa Ajili ya Ukombozi wa Angola ambacho kimeshinda viti 191 katika ya viti 220 vya bunge. Angalia baadhi ya maoni.
Angola: Uchaguzi Katika Picha
Waangola wako katika uchaguzi kwa mara ya kwanza katika miaka 16 - uchaguzi bado unaendelea Jumamosi hii katika vituo 320 jijini Luanda. Mpaka sasa, hakuna matukio yoyote yaliyoripotiwa, na moyo wa utu umedumu, kama ilivyoangaliwa na mpiga picha Jose Manuel da Silva.